Hayo yamejiri baada ya kujiri mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Kishia wa Houth ambao walifanikiwa kuzingira kwa muda makao makuu ya televisheni ya taifa mjini San’aa. Zaidi ya watu 100 wamefariki dunia nchini Yemen toka Alkhamisi kutokana na mapigano hayo.
Wafuasi wa Harakati ya Ansarullah na waungaji mkono wao wamekuwa wakifanya maandamano mjini Sana'a kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa wakitaka serikali mpya iundwe.
